Mtazamo wa Uturuki Mashariki ya Kati

Mtazamo wa Uturuki Mashariki ya Kati

Mtazamo wa Uturuki Mashariki ya Kati

Rais wa Jamhuri ya Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan alitetekeleza ziara ya Marekani ambapo alikutana na mwenzake wa nchi hiyo rais Donald Trump.Leo katika kipindi cha Mtazamo wa Uturuki Mashariki ya Kati tutazungumza kuhusu athari za ziara ya rais Erdoğan Marekani na masuala waliojadili na rais Donald Trump.

 

Kutoka Chuo kikuu cha Atatürk Kitengo cha Mahusiano ya kimataifa Dkt.Cemil Doğaç İpek anatoa tathmini ya kipindi chetu cha leo.

 

Rais Recep Tayyıp Erdoğan ametekeleza ziara rasmi katika nchi ya Urusi,China ,India na mwishowe akamalizia na Marekani.Kwa mara ya kwanza Erdoğan na Trump walifanya mkutano wa ana kwa ana .Matukio ya mkutano baina ya viongozi hawa wawili yalifuatiliwa kwa ukaribu na jumuiya ya kimataifa,na mjadala wao unaonekana kuboresha uhusiano wa kikanda baina ya nchi hizi mbili.

Kutoka maelezo kutoka viongozi hao wawili,yaliashiria kuwa wapo tayari kuungana pamoja na kuboresha uhusiano kati yao huku wakitupilia mbali hali zozote za mtafaruku na mvutano.Hata hivyo kuhusu suala tawi la PKK lililopo Syria la YPG inaonekana kuwa bado walikuwa wanatofautiana kimawazo .Lakini cha muhimu ni kuwa kuna maendeleo ikilinganishwa na uhusiano wa Uturuki hapo awali na serikali ya Obama .

Ni wazi kuwa Marekani haitobadili wazo kuhusu kuunga mkono kundi la YPG lililopo Syria ambalo ni tawi la kundi la kigaidi la PKK.Marekani inaonekana kuendelea na mpango wake wa kutoa msaada wa silaha kwa YPG.Pia ni wazi kuwa Marekani imetoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu kushirikiana na YPG katika operesheni dhidi ya DAESH Raqqa.Baada ya kukombolewa kwa Raqqa YPG haitoruhusiwa kutawala eneo hilo,Marekani imeipa hakikisho Uturuki kuwa eneo hilo halitakuwa mojawapo ya mwantya wa PKK ,hata hivyo Uturuki haina uhakika kuhusu hilo kwa kuwa na uzoefu waliopata Munbij.Katika jibu lake kuhusu suala hilo rais Erdoğan alisema kuwa kuwa lengo la Uturuki ni kuondoa vitisho vyote vya kigaidi karibu na nchi yake na kwamba wao watafanya hatua ambazo zitakuwa kwa sababu ya usalama wa Uturuki na kwamba hawatangoja kuuliza yeyote kuhusu hatua watakazochukua .Kila mara Uturuki na Marekani hupingana katika sera zitakazotumika kupambana na makundi ya kigaidi.Ni kwa sababu ya kutokuwa na lengo moja kuhusu suala hilo kumeendelea kuwa na vurugu zaidi Mashariki Ya Kati.

Leo hii mataifa mengi ya magharibi yanajaribu kuonyesha tofauti baina ya YPG Na PKK.Lakini ukweli ni kwamba YPG ni sehemu ya kundi la kigaidi la PKK lililopo Syria.Kuna ishara ambazo zinathibitisha ukweli huu.Karibu ya mwaka mmoja uliopita naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Ashton Carter aliwahi kuulizwa ikiwa YPG ya Syria ni tawi ya PKK alisema’NDIO’.

Hivi karibuni PKK/YPG imechapisha makala malum katika mojawapo ya majarida muhimu ya Marekani ya The Atlantic.Mwandishi wa makala haya ni balozi wa zamani wa Marekani nchini Syria ,Robert Ford.Katika makala hayo Ford anasisitiza kuwa PKK ilianzishwa katika milima ya Kandil mnamo mwaka 2003.Aidha anaelezea kuhusu uhusiano baina ya PKK,KCK,PYD/YPG.Kulingana nam akala mengine ya hapo awali katika jarida la Wall Street Journal PYD inakiri kuwa tawi la PKK.Ford anaelezea kuwa ni hivi karibuni tu ambapo seriakli za Trump na Obama zinasema kuwa PYD/YPG hazina uhusiano na PKK.Mpango wa PYD kuchukua udhibiti wa kanda ya kaskazini mwa Syria ni hatua ya kiukarabati ili kufanikisha mashambulizi ya PKK dhidi ya Uturuki.Pia anaelezea kuwa wapiganaji wanaopewa mafunzo Kaskazini mwa Syria wanatumiwa katika kutekeleza mashambulizi Istanbul ,Ankara na Bursa .Kwa kuwa Marekani imeamua kuchanganya siasa zake na sera zake katika kupambana na ugaidi kwa kuungana na kushirikiana na makundi ya kigaidi inaifanya kukosa imani kutoka nje .   

Hata hivyo kando na suala hilo ziara ya Marekani ya rais Erdoğan ilikuwa na matokeo mazuri.Kwanza kabisa hali isiyoeleweka kuhusu uhusiano wa Marekani na Uturuki ilibainishwa kwa mara ya kwanza ,uhusiano baina ya nchi hizo mbili umeletwa sawa.Hii ni ishara kuwa ni ukurasa mpya kwa Uturuki na Marekani.Hata hivyo kuna maswali yanatokea kufuatia kuwekwa sawa kwa mahusiano haya,je kutakuwa na ushirikiano sasa baina ya nchi hizi mbili bada ya hapo?Kwa sasa ni vigumu kutoa jibu ,ushirikiano baina ya nchi hizi mbili utategemea hatua za kijeshi hasa katika maendeleo ya nchi ya Syria.Habari Zinazohusiana