Makala ya Ibrahim Kalın

"Tukifanikisha amani, usawa na usafi katika nyonyo zetu ndivyo tutaweza kuhamasisha usawa na haki katika siasa na uchumi"

Makala ya Ibrahim Kalın

Kunao uwezekano wa kuwa na dunia iliyo na usawa?

Katika wiki tano zilizopita rais Recep Tayyıp Erdoğan ameweza kufanikisha ziara za kifiplomasia katika nchi ya India, Urusi, China na hatimaye Marekani.

Mwisho kabisa alihudhuria kongamano la NATO nchini Ubelgiji .

Katika mkutano huo masuala muhimu yaliyopewa kipaumbele ni mbinu za kutafuta ustawi, amani na muelekeo wenye usawa baina ya uhusiano wa kikanda na kimataifa katika kipindi ambacho dunia inakumbwa na migogoro na vurugu.

Kutoka Ankara hadi New Delhi , kuvuka kwena Washington na hata Moscow na Beijing kumekuwa na hofu moja kuhusu kuendelea kwa vita nchini Syria, ugaidi kuzuka kimataifa , harakati za kiubaguzi na mabadiliko ya hali ya anga .

Hata hivyo ifahamike ya kwamba vurugu na migogoro ya sasa katika nyanja za kimataifa  imesababisha na siasa na uchumi.Kutokuwa na usawa baina ya mataifa imepelekea kuwa na ongezeko la mvutano na utovu wa maelewano baina yao.Vita vya Syria ni mfano mzuri wa mgogoro huu wa kimataifa, hadi kufikia sasa Syria imekuwa katika dimbwi la vita na umwagikaji damu kwa takriban miaka 6.Maelfu ya watu nchini humo wamepoteza maisha yao na kupelekea kuwa mojawapo ya vita vibaya zaidi katika historia ya karne ya 21.Cha kusikitisha ni kwamba vita hivi havitoisha hadi pale waendeshaji wanahakikisha wametimiza ajenda na matakwa yao.

Kwengineko barani Afrika matatizo ya uhaba wa chakula, umasikini, ufisadi na unyanyasaji hayataisha sio kwa sababu Afrika haina uwezo bali kwa sababu Afrika inatumika kama eneo la kazi duni, uharibifu ili kuendeleza utajiri katika mataifa ya magharibi.Dunia sasa inakumbwa na mgogoro mbaya zaidi wa wakimbizi na mataifa tajiri hayataki kuona tatizo hilo kuwa kuu isipokuwa washuhudie jambo hilo lipo milangoni mwao.Pengo lililopo baina ya maskini na tajiri laendelea kuwa kubwa sio kwa sababu haliwezi kutatulika bali kwa sababu hamna nia ya kutaka kubadili hali hiyo itakayopeleka mabadiliko muhimu duniani.

Dunia ya sasa inashuhudia utajiri mkuu na maendeleo tata katika historia ya mwanadamu. Dunia yetu haipati matatizo kutokana na ukosefu wa teknolojia wala kutokuwa na njia mbadala za kutatua matatizo bali inapata tabu kutokana na tatizo kuu zaidi;ukosefu wa maana, muelekeo na sababu katika nyanja za kimataifa.Vurugu na migogoro duniani ni kioo cha kuwa na ukosefu wa usawa na mpangilio ambayo inaashiria kwa undani sisi kama watu binafsi vitu tunavyotaka na ni watu wa aina gani tunaendelea kuwa .

Hekima ya hapo jadi inaashiria ya kuwa amani na mpangilio katika dunia ya nje haiwezi kufanikishwa isipokuwa mwanzo amani na usawa ndani yetu sisi wenyewe inahakikishwa.Hii ina maana kuwa kuna usawa ambao sharti uafikiwe baina ya dunia ya nje na ya ndani.

Hii ndiyo kwa sababu mwanafalsafa Plato alielezea falsafa ya usawa .Kazi ya mwanafalsafa ni kuonyseha jinsi ya kufanikisha usawa baina ya dunia ya nje na ndani.Usani wa hekima ni kutambua njia za kusawazisha usawa katika kila nyanja na ufahamu.Plato katika uchambuzi wake anaashiria usawa katika muziki na anafahamisha ili kufanikisha kazi hiyo sharti muundo, usawa , mpangilio na mfuatano au uzani wa muziki uzingatiwa kwani hizo ndio nguzo muhimu za muziki wowote ulio mzuri.Changamoto kuu ni kusawazisha mpangilio na uzuri bila ya kwenda kinyume na matakwa yetu ya amani na uhuru.

Usawa ni mfumo ambao sharti uwe na vigezo vya ukweli na haki.Hamna mfumo wenye uwongo na uhalifu utakaoweza kuhamasisha usawa na mpangilio mzuri.Vile vile haki ni kigezo muhimu cha kuhamasisha amani katika jamii yoyote ile .Jamii huwa na upendo na amani iwapo kila mtu atatekeleza jukumu lake kwa usawa na haki kwa kuelekea upande mmoja.Vile vile mwili wa binadamu huwa sawa ikiwa kila kiungo na sehemu yake itafanya kazi yake kulingana na maumbile yenyewe.

Katika utamaduni wa kiislamu usawa ni uti wa mgongo wa uumbaji wa dunia.Usawa ndio unapelekea umoja wa dunia .Pia ni kigezo muhimu katika maisha yetu ya ndani na kinyume na hicho inapelekea vurugu na ukosefu wa amani katika roho zetu.

 

 Habari Zinazohusiana