Kuhusu TRT VOT

KUHUSU TRT

HISTORIA

Matangazo ya nje ya Uturuki ya kwanza yalianzishwa na shirika la Ankara Radio Corporation tarehe 8 Januari mwaka 1937. Matangazo haya yaliyoanzishwa kwa lengo la kutatua tatizo la Hatay, yalikuwa yakipeperushwa kwa lugha ya kiarabu kuwasilisha ujumbe uliotolewa na Waziri Mkuu wa kipindi hicho İsmet İnönü.

Kufatia kuenea na kusambaa kwa matangazo ya kijamii katika mkoa wa İskenderun, Syria na maeneo jirani, taarifa kwa lungha ya kiarabu zikaanzishwa na kituo cha İstanbul Radio Corporation. Kwa kweli utangazaji wa taarifa kwa lugha ya Kiarabu ulikuwa sio wa kawaida, na ulifikia kikomo muda mfupi baada ya tatizo la Hatay kutatuliwa.

Matangazo kwa lugha ya Kituruki, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani yalianza tarehe 28 Oktoba mwaka 1938.

Wakati wa vita vya pili vya dunia, ‘’Short Wave Ankara Radio’’ ilipata mvuto mkubwa kutoka kwa umma kutokana na juhudi zake za utangazaji miongoni mwa vituo vyengine vya redio duniani.

Ni miaka hio kuanzia 1943 mpaka 1949 ambapo kituo hicho cha redio kilipopata fursa ya kurusha matangazo Marekani, Magharibi na Mashariki ya mbali pamoja na Australia.

Kipindi chengine chenye umuhimu ni wakati Uturuki ilipojiunga na NATO kati ya mwaka 1949 na 1958 na kutuma wanajeshi katika vita vya Korea na kuimarisha uhusiano na Magharibi.

Tangu kuanzishwa kwake, redio hii imekuwa ikifanya matangazo yake ya nje kwa jina la ‘’Short Wave Ankara Radio’’ hadi kufikia Januari mwaka wa 1963, ndipo matangazo yote yamekuwa yakifanywa kwa jina la ‘’Voice of Turkey’’ (VOT) hadi kufikia sasa.

Baada ya idhaa ya Redio na Televisheni ya Kituruki (TRT) kuanzishwa tarehe 1 Mei mwaka 1964, VOT ilianza utendaji kazi katika kitengo kimoja chini ya TRT.

 

 

Voice of Turkey

Hadi waleo, Voice of Turkey imekuwa ikipeperusha matangazo ya TRT ya redio za nje.

 

Katika mpangilio wake wa idara ya matangazo ya nje, VOT inarusha matangazo kila siku kwa lugha 29 zikiwemo Kituruki, Kijerumani, Kialbenia, Kiarabu, Kiazeri, Kibosnia, Kibulgaria, Kikroshia, Kichina, Dari, Kifarsi, Kifaransa, Kigogia, Kingereza, kihispania, Kitaliano, Kikazakhistan, lugha ya Kirgizistan, ya Hungary, Macedonia, Pashtun, Uzbekistan, Kiromania, Kirusi, Kiserbia, lugha ya Tataristan, Turkmenistan, Kiurdu na Kigiriki.

VOT inahudumia dunia nzima kupitia mawimbi ya usambazaji, satelaiti na mtandao. Ina mipango ya kupanua huduma zake ili iweze kuwafikia wasikilzaji wengi zaidi kupitia njia za nyuzi za FM za hapa nchini.

Kutokana na uzingatiaji wa kanuni na uadilifu, ufasaha na usahihi wa matangazo yake, VOT inazidi kuboresha utangzaji wake kwa vipindi vya kuvutia vinavyolenga umma kwa ujumla pasi na kukagua umri au jinsia, na kuimarika kama kituo bora cha kuaminika kwa taarifa zake.

Nchi ya Uturuki na raia wa Kituruki kwa ujumla huvuta taswira kupitia vipindi vya taarifa za habari, utamaduni na sanaa, na burudani ya muziki. Kwa kutekeleza sera ya Uturuki ya kudumisha uhusiano mzuri na nchi jirani na kuhimiza kuwepo kwa ushikamano baina ya mikoa, matangazo husisitiza amani na ushirikiano.