Zimbabwe kufanya uchaguzi mwezi Julai

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini Zimbabwe mnamo Novemba, uchaguzi wa rais unatarajia kufanyika Julai.

Zimbabwe kufanya uchaguzi mwezi Julai

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini Zimbabwe mnamo Novemba, uchaguzi wa rais unatarajia kufanyika Julai.

Rais Emmerson Mnamgagwa amesema kuwa uchaguzi wa uhuru na wa haki utafanyika Julai.

Mnamgagwa amesema kuwa uchaguzi huo utakuwa wa amani na wa uwazi,

"Uchaguzi huu utakuwa uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia katika nchi yetu baada ya udikteta wa muda mrefu," alisema

Mnamgagwa amesisitiza kuwa uchaguzi huu utasaidia kuboresha mahusiano na Ulaya yaliyokatwa na rais wa zamani Robert Mugabe.Mnamgagwa amesema atawaalika waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya kutizama uchaguzi huo.

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini Zimbabwe mnamo Novemba, Robert Mugabe, aliyekuwa katika mamlaka kwa miaka 37, alijiuzulu na Emmerson Mnangagwa akachukua nafasi yake.Habari Zinazohusiana