UN yasema zaidi ya watu milioni 5 wanahitaji msaada nchini Sudan

Umoja wa Mataifa umetangaza  kuwa watu zaidi ya milioni 5 nchini Sudan wanahitaji usaidizi wa kibinadamu

UN yasema zaidi ya watu milioni 5 wanahitaji msaada nchini Sudan

Umoja wa Mataifa umetangaza  kuwa watu zaidi ya milioni 5 nchini Sudan wanahitaji usaidizi wa kibinadamu na karibu watoto milioni 2.5 huko hupata ugonjwa kila mwaka kutokana na utapiamlo.

Idadi ya watu wenye mahitaji nchini Sudan imeongezeka kwa 700,000 ikilinganishwa na mwaka jana hadi milioni 5.5.

Ofisi ya Sudan  ya Umoja wa Mataifa ya Udhibiti wa Maendeleo ya Ubinadamu (OCHA) imesema kuwa maafa ya asili kama mafuriko na ukame yameathiri vibaya usalama wa chakula na maisha ya watu walio katika mazingira magumu nchini.

Kwa mujibu wa habari kila mwaka, watoto karibu milioni 2.5 huugua kutokana na utapiamlo  na karibu 700,000 wao huathirika sana.

Wakati uzalishaji wa kilimo ukiwa umeboreshwa mwaka wa 2017,bei kubwa ya chakula imezidi kuwa changamoto.

 Habari Zinazohusiana