Ushirikiano baina ya Uturuki na Afrika

Jitihada na mapambano ya chama cha ANC katika kutawala

Ushirikiano baina ya Uturuki na Afrika

Jitihada na mapambano ya chama cha ANC katika kutawala

Imechambuliwa na Abdoulaye Ibrahim Bachar

Chama cha Mandela nchini Afrika Kusini ANC, kilichotawala baada ya ubaguzi wa rangi yani ”Apatheid Policy” kimekumbwa na matatizo mengi ndani ya miaka ya hivi karibuni. Jacob Zuma aliyeingia madarakani baada ya migogoro ya ndani kwa ndani mwaka 2008 alilazimika kujiuzulu siku chache zilizopita kutokana na mgogoro wa kisiasa.Mgogoro wa siku nyingi kati ndani ya chama ulisababisha chama cha ANC kupoteza umaarufu wake.Hali iliyopelekea chama hicho kupoteza baadhi ya sehemu wakati wa uchaguzi  2016. Katika uchaguzi wa mitaa uliofanyika mwaka 2016, ANC ilipoteza Johannesburg na Pretoria, miji miwili  muhimu ya Afrika Kusini. Ilianza kujadiliwa baada ya kipindi cha uchaguzi kuwa kwa mara ya kwanza chama cha ANC kimeanza kupoteza nguvu yake.

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini humo kimeongezeka hadi 28% katika miaka ya hivi karibuni, hali iliyosababishwa na matatizo ya ANC. Aidha, baada ya Nelson Mandela  chama kimeonekana kuanza kupoteza uaminifu wake kwa watu .Mapambano na matatzio ndani ya chama chenyewe yamepelekea chama kujipaka matope.

Thabo Mbeki, ambaye aliingia madarakani baada ya Nelson Mandela, alijikuta katika mgogoro na baadhi ya viongozi wa ANC ambao hawakufurahishwa na siasa alizokuwa akizifanya. Mbeki, alichaguliwa 1997 wakati wa mkutano wa ANC uliofanyika  Mafikeng akiungwa mkono na  Nelson Mandela,mgombea Cyril Ramaphosa na vilevile Jacob Zuma.Zuma baadaye alichaguliwa kuwa makamu wa rais lakini muda Mbeki alimuondoa Zuma katika nafasi hiyo kutokana na khashfa za ubakaji na ufisadi.

Baadaye, katika uchunguzi dhidi ya Jacob Zuma, ilisemekana  kuwa Thabo Mbeki alikuwa akiishinikiza mahakama. Hili lilileta mgawanyiko ANC kutokana na mashindano ya madaraka kati ya Mbeki na Zuma. Kwa msingi huu, wafuasi wa Zuma katika ANC wakamshtaki Thabo Mbeki kuwa kiongozi mwenye kutumia mabavu na kutishia umoja wa chama. Pia walijaribu kumdhoofisha Thabo Mbeki kwa umma kwa  kufanya propaganda katika vyombo vya habari.

Desemba 18, 2007 katika mkutano wa ANC nchini Afrika Kusini, chama chenye nguvu zaidi  Afrika Kusini, vilikuwepo na Vyama vya Wafanyakazi ,ambapo kura zilipigwa na Zuma akapata silimia 60 ya kura hizo jambo lililomfanya Thabo Mbeki kufukuzwa na Zuma kufanywa kiongozi wa chama hicho. Mnamo Septemba 2008, Kamati ya Taifa  (NEC) ya ANC, İlitoa wito wa kujiuzulu kwa Thabo Mbeki kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama kwa ujumla. Mbeki alipoteza watu wa kumuunga mkono ANC,na hivyo akaishia kujiuzulu. Mnamo Aprili 6 mwaka 2009 Zuma alifunguliwa kesi ya rushwa. Baada ya hapo, Mei 6, Jabob Zuma alichaguliwa kuwa rais. na hivyo basi ikaonekana kuwa , ugomvi kati ya Zuma na Mbeki  ni wa faida kubwa na neema kwa Jacob Zuma.

 Mnamo Juni 2014,Jacob Zuma alimleta mpinzani wa zamani wa Thabo Mbeki, Cyril Ramaphosa kuwa makamu wa rais. Kabla ya hapo licha ya kupewa msaada na Nelson Mandela chama cha ANC hakikumchagua Ramaphosa mwaka 1997..Baada ya hapo Ramaphosa akaamua kuachana na siasa na kuendelea na masiha yake kama mfanyabiashara. mpaka hapo 2014.

Ramaphosa aliingia orodha ya wafanyabiashara tajiri nchini Afrika Kusini.Muda mfupi baada ya Ramaphosa kurudi katika siasa,Zuma alianza kupoteza nguvu katika chama cha ANC.Alikumbwa na ajenda mpya za khashfa na rushwa  na kusababisha mgogoro ndani ya chama.Wapinzani wa Zuma ANC walishirikiana na vyama vya upinzani kumpiga vita Zuma. Hasa chama cha Mmusi Maimane's Democratic Alliance (DA) na Julius Malema's Economic Freedom Warrior na Julius Malema Economic Freedom Fighters (EFF) ni kati ya vyama vilivompinga vilivyo Zuma.Licha ya hayo yote Jacob Zuma aliweza kuendelea kukidhibiti chama cha ANC.

Hata hivyo, Desemba 18, 2017 Zuma alimleta mke wake wa zamani Nkosazana Dlamini lakini akashindwa kuchaguliwa dhidi ya makamu wa rais Cyril Ramaphosa.Hali hii ilizua wasiwasi kuwa Zuma ana mpango wa kufunga kesi zake za rushwa kwa kutaka kumchagua  mke wake wa zamani.

Baada ya Cyril Ramaphosa kuwa mwenyekiti wa ANC,hali ilianza kuwa mbaya kwa Zuma.Miezi miwil baada ya kuanza kazi Ramaphosa ,Jacob Zuma alilazimishwa na chama kujiuzulu.Tayari sasa chama kinajitaarisha kwa uchaguzi wa mwaka 2019 kwani kutokana na mgogoro wa ndani kwa ndani chama kinaweza kupoteza nguvu yake.

Kulikuwa na wafuasi wa Zuma katika chama cha ANC na wafuasi wa Ramaphosa.Kumekuwa na mvutano kati ya pande hizo mbili..Hata katika baadhi ya magazeti iliandikwa kuwa wanachama wawili waligombana katika mji wa Johannesburg kabla ya kujiuzulu kwa Zuma.

Baada ya hatua kuchukuliwa na uchunguzi kufanyika ilionekana wazi kuwa Zuma ankabiliwa na mashtaka mengi na hivyo chama kikaungana na kumtaka ajiuzulu.Katibu mkuu wa ANC na aliyekuwa shabiki mkubwa wa Zuma, Ace Magashule alikutana na Ramaphosa Februari 12 na kutangaza kuwa chama kinamtaka Jacob Zuma aachie ngazi.

Hata hivyo Zuma alienda katika televisheni na kuweka mgomo kuwa hatajiuzulu.Zuma alitoa uamuzi wake baadae kuwa amejiuzulu na akasema kuwa hajafurahishwa na uamuzi wa chama chake.Alisema alifanya hivyo kwa kukiheshimu chama.

Miaka 9 iliyopita Zuma aliingia madarakani kwa kumpiku Thabo Mbeki na sasa ametolewa na Ramaphosa.Baada ya kujiuzulu kwake familia ya Gupta nchini humo imeanza kushambuliwa.Wananchi wanasubiri kutizama ni hatua gani zitachukuliwa dhid ya rushwa toka kujiuzulu kwa Zuma siku chache zilizopita.

 Habari Zinazohusiana