Ushirikiano baina ya Uturuki na bara la Afrika

Safari ya George Weah

Ushirikiano baina ya Uturuki na bara la Afrika

Wiki iliyopita katika taifa la  Afrika Magharibi, Liberia, watu waliadhimisha mwaka mpya kiaina yake. Hii ni baada ya ushindi wa nyota wa mpira wa Afrika wa Georg Weah katika mzunguko wa pili wa uchaguzi wa urais mnamo Desemba 26.

Wakati matokeo ya uchaguzi yakitangazwa, wananchi katika mji mkuu wa Monrovia walionekana wakisherehekea ushindi wa George Weah na kujawa na matumaini ya kuwa na Liberia mpya.

 Liberia likiwa ni taifa lenye sifa ya kupata uhuru wa kwanza barani Afrika,ni taifa ambalo lilikombolewa na Sammuel Deon(1980-1990) dhidi ya wakoloni wa ”Congos” kutoka Marekani.

Sammuel Deon aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi. Wakoloni hao waliunda mfumo wa unaguzi wa rangi ”apartheid policy” na kuwanyima wazawa haki zao za msingi.

Pia katika miaka 1989-2003 kumekuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo watu zaidi ya elfu walipoteza maisha yao na kuleta hali mbaya ya kiuchumi.

Maisha ya waliberia yalizidi kuwa magumu baada ya mlipuko wa ugonjwa 2014. Mnamo 2016, kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (Minul) kilijiondoa nchini humo.

Hali hii ilisababisha elimu kuwa ghali na mfumuko wa bei nchini. 64% ya idadi ya wananchi nchini humo wapo chini ya kiwango cha umasikini na idadi ya watoto kati ya umri wa miaka 14 na 25 ambao humaliza elimu ya msingi ni 62%.

 Sababu iliyomfanya George Weah kuwa mgombea maarufu ni kwamba wakati wa kampeni ya uchaguzi aliahidi kupambana na masikini. Jambo hili lilimfanya George kuwa shujaa wa watu.

Kama watoto wengi wa Liberia, Geoge Weah hakumaliza shule. Alilelewa na bibi yake na kuishi maisha duni.

Historia ya maisha yake ilitoa tumaini kwa vijana wa Liberia. George, ambaye aliishi maisha ya umaskini wakati wa ujana wake, alikuwa akitumia muda mwingi akicheza mchezo wa mpira wa miguu wa kwenye simu kama kipa wakati akitengeneza simu za watu. Maisha ya George, yalibadilika pale alipochaguliwa na kocha wa AS Monaco Arsene Wenger mwaka 1988 wakati akiichezea  klabu Cameroon akiwa na umri wa miaka 20.

Kwa miaka 14 George Weah amekuwa akichezea klabu za PSG, Milan AC, Chelsea, Manchester City na Olympique de Marseille na kushinda "Ballon d'Or" 1995 akiwa ni mwansoka pekee wa Afrika kushinda tuzo hio.

 Wakati akiwa katika soka nchi ya Liberia ilikuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Wakati huo Umoja wa Mataifa ulialikwa kuwakomboa wa Liberia, na nyumba ya george Weah iliwaka moto huko Monrovia na binamu zake wawili walichukuliwa mateka.

Pia alikuwa mtu wa kawaida ambaye hakushiriki katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, na hii ikachangia kwa George Weah kuwa maarufu sana. George Weah aliishi Miami, Marekani baada ya kazi yake ya uwanasoka. Katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 2005, wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza mwaka 2003, George Weah akawa mgombea wa urais baada ya kuombwa na watu wake wa karibu.

George Weah, ambaye alipata 40% ya kura dhidi ya Ellen Johnson Sirleaf, mgombea wa Umoja wa Chama (UP), alipoteza uchaguzi. Kwa mara ya pili tena hakuweza kupata ushindi  dhidi ya mgombea huo,  katika uchaguzi wa 2011.

Mpinzani wa George Weah, Ellen Johnson  alikuwa mwanafunzi wa Harvard na amewahi kufanya kazi muhimu katika Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia.

Baada ya kukashifiwa na wapinzani wake kuwa hana elimu ya kutosha George Weah alipata diploma yake katika idara ya biashara na diplomasia nchini Marekani kati ya 2011 na 2014 na kuchaguliwa kama kiongozi wa diplomasia wa Monrovia mwaka huo huo.

George Weah aliyeshindwa uchaguzi mara mbili akiwa mgombea wa Congress for Democratic Change (CDC) alitangazwa kama mshindi wa uchaguzi nchini humo Desemba 28 yani Alhamisi iliyopita.kwa mujibu wa matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi George Weah 51 alipata  61.5%, wakati mpinzani wake Joseph Noaka 73 akiwa amepata 38.5% ya kura. Katika mzunguko wa pili George Weah, aliungwa mkono na Prince Johnson maarufu kwa kumuua rais wa zamani Doe Sammuel na pia akasaidiwa na mke wa zamani wa Charles Taylor,aliyepewa miaka 50 jela kimakosa na mahakama ya kimataifa.

George Weah, ambaye amepata imani na heshima ya watu, anaonekana kama matumaini kwa wananchi maskini.Wananchi humuita  "Mister George" na wakati wa kampeni za uchaguzi aliahidi kupambana dhidi ya rushwa, elimu ya bure, ukosefu wa ajira, masuala ya mahitaji ya msingi kama vile kuboresha mfumo wa afya ya umma na miundombinu na ameahidi kuwa mstari wa mbele.

George Weah aliyetokea katika masiha ya umaskini amekuwa akisema kuwa amekulia katika maisha ya kawaida na hivyo atapigana dhidi ya umaskini kwa wananchi wake wa Liberia.

Kumbuka, watu wa Liberia katika uchaguzi wa 2005 walikuwa na matumaini sana kwamba Ella Johnson alikuwa kama George Weah leo.

Wanawake wafanyabiashara nchini wameanzisha shirika la "Soko la Wanawake" na kumuunga mkono Ella Johnson wakati akiwa mgombea. Hata hivyo, mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais barani Afrika Ella Johson hakufanya kitu chochote mbali na kuleta amani ambayo ilipatikana katika mihula yake miwili ya mwisho na vilevile kukuza uchumi.

Matarajio ya watu kutoka kwa Geroge Weah, ambaye ameanza rasmi Januari 2, ni makubwa. Mara baada ya ushindi wake aliandika kwenye akaunti ya Twitter "Ninahisi sana hisia za watu na nina furaha”.

Leo ninapima umuhimu na wajibu wa kazi yangu kubwa. Njia ya mabadiliko imefunguliwa. Ingawa Liberia ina utajiri wa almasi, mpira, chuma, madini ya thamani na mitende ya mafuta, asilimia 60 ya watu wanaishi chini ya dola mbili kwa siku. Kwa miaka mingi, uchumi wa nchi umechukuliwa na kampuni ya Marekani FIRESTONE.

Ili watu wa Liberia, ambao wako katika matarajio ya juu kukidhi mahitaji, Weah anahitaji kuchukua hatua za haraka katika ustawi wa jamii.

Hata hivyo, kutokana na kupungua kwa misaada ya kigeni inayoingia nchini na kupungua bei za malighafi, haitakuwa rahisi kuboresha uchumi wa nchi. Kwa hiyo ni wazi kwamba George Weah anatarajia kuwa na kazi ngumu.Habari Zinazohusiana