Upinzani walaani uahirishaji wa uchaguzi DRC

Chama cha upinzani nchini Congo kimelaani uamuzi wa tume ya uchaguzi kusogeza uchaguzi wa nchi hiyo mpaka hapo 2019.

Upinzani walaani uahirishaji wa uchaguzi DRC

Chama cha upinzani nchini Congo kimelaani uamuzi wa tume ya uchaguzi kusogeza uchaguzi wa nchi hiyo mpaka hapo 2019.

Mwenyekiti wa chama cha upinzani Batumona Kandi amesema kuwa upinzani umegundua kuwa kiongozi wa tume ya uchaguzi anashirikiana katika njama na rais Kabila katika kuhakikisha uchaguzi haufanyiki nchini humo.

Hata hivyo bwana Nanga amesema kuwa upinzani utapigana vilivyo kuhakikisha uchaguzi unafanyika nchini DRC.

Kwa mujibu wa habari,uchaguzi ulikuwa unapaswa kufanyika mwaka jana na ghafla umeahirishwa mpaka mwaka 2019.

Kiongozi huyo wa upinzani amesema kuwa haina maana kwa uchaguzi huo kusogezwa mbele.

Upinzani umeahidi kuhakikisha unapigania uchaguzi kufanyika ndani ya siku 504.

Muhula wa Kabila kutawala uliisha Desemba mwaka jana lakini rais huyo amegoma kutoka madarakani akisema kuwa nchi hiyo bado haipo tayari kwa uchaguzi mpya.

 


Tagi: uchaguzi , Congo

Habari Zinazohusiana