Israel kuwekeza katika sekta ya Nishati barani Afrika

Israel kufanya uwekezaji wa dola bilioni moja katika nishati ya jua magharibi mwa Afrika

Israel kuwekeza katika sekta ya Nishati barani  Afrika

Israel na mataifa ya shirika la ECOWAS kanda ya magharibi wa Afrika imetia saini mkataba wa kufanya uwekezaji wa nishati ya jua katika mataifa 15 kwa muda wa miaka 4.

Uwekezaji huo utaigharimu Israel jumla ya dola bilioni 1.

Mkataba huo ulitiwa saini siku ya Jumamosi kabla ya kuanza kongamano la viongozi wakuu katika nchi washirika wa ECOWAS katika mji mkuu wa Monrovia nchini Liberia.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alialikwa kuhudhuria mkutano huo.

Balozi wa Israel magharibi mwa Afrika Paul Hirschson aliambia shirika la habari la Anadolu kwamba Israel inaipa umuhimu mkubwa uhusiano mwema baina yake na Kanda ya magharibi ya Afrika .

Masuala ya mapambano dhidi ya ugaidi, mabadiliko ya hali ya anga , uongozi na maendeleo ndiyo yaliyojadiliwa katika kongamano la ECOWAS.

 

 Habari Zinazohusiana